Online

Wednesday, February 22, 2017

UEFA: Manchester City 5-3 Monaco: Pep Guardiola mguu moja robo-fainali UCL

MANCHESTER City ilitoka nyuma maa mbili na kupata faida ya mabao mawili baada ya mchezo mzuri wa Champions League hatua ya mtoano dhidi ya Monaco uliopigwa uwanja wa Etihad.
Katika usiku wa kushangaza, vijana wa Pep Guardiola walianza kwa kusuasua kabla ya kuamka na kujihakikishia wanaifuata Monaco kwenye mchezo wa marudiano wakiwa na mabao ya kutosha.
Raheem Sterling alitangulia kuifungia Manchester City dakika ya 26 baada ya kazi nzuri ya Leroy Sane lakini Monaco walithibitisha kitisho chao kwa kuongoza kabla ya mapumziko kupitia kwa Radamel Falcao na Kylian Mbappe.
Falcao akakosa mkwaju wa penalti ambayo iliokolewa na Willy Caballero baada ya mapumziko kabla ya kipa wa Monaco Danijel Subasic kufanya makosa yaliyomruhusu Sergio Aguero kusawazisha.
Mcolombia Falcao, katika kiwango chake bora baada ya kuchemsha alipokuwa kwa mkopo Manchester United na Chelsea, akamzidi ujanja Caballero na kuifungia Monaco bao la tatu - lakini hii ilikuwa ishara kwa City kujipanga.
Aguero - ambaye alikataliwa penalti kipindi cha kwanza baada ya kuchezewa vibaya na Subasic - alisawazisha kwa mara nyingine kabla ya John Stones kuifungia City bao la nne dakika ya 77.
Nyota wa mchezo Sane akafunga bao la tano zikisalia dakika nane - lakini uimara wa Monaco katika kushambulia maana yake ni kuwa mchezo wa marudiano utakuwa mgumu sana.

Monaco inaongoza orodha ya mabao - dondoo

  • Man City ilifunga mabao matato kwenye mchezo wa Champions League kwa mara ya pili (mwingine ulikuwa mabao 5-2 v CSKA Moscow 2013, ukiondoa hatua ya kufuzu).
  • Mchezo huu ni mara ya kwanza mabao manane yamefungwa kwenye mchezo wa kwanza wa Champions League hatua ya mtoano.
  • Raheem Sterling amehusika na mabao 10 kwenye mechi tisa za Champions League alizoanza (mabao matano, assist tano).
  • Kylian Mbappe ni mchezaji kinda wa pili kutoka Ufaransa kufunga kwenye Champions League, akitanguliwa na Karim Benzema (miaka 17 na siku 352) ambaye aliifungia Lyon dhidi ya Rosenborg Disemba 2005.
  • Falcao amefunga mabao mengi Etihad (2) sawa na mechi 15 alipokuwa Old Trafford akiwa na Manchester United.
  • Fabinho litoa assist nyingi kwenye mchezo huu (2) zaidi ya alivyowahi kufanya katika mechi  15 zilizopita kwenye Champions League (1).
  • Bao la kwanza la Sergio Aguero lilikuwa bao la 200 kwa Manchester City la Europe (mabao 203 mpaka mwisho wa mchezo huu). Amefunga mabao matano katika mechi tatu zilizopita za Champions League Etihad.
  • Manchester City imeokoa penalti zote tano zilizopita kwenye Champions League (mbili zimeokolewa na Caballero, tatu ziliokolewa na Joe Hart).
  • Monaco ni timu inayoongoza kwa mabao miongoni mwa timu za ligi kuu tano Europe msimu huu kwenye mashindano yote ikiwa na mabao 111.
  • Kulikuwa na kadi za manjano 10 - nyingi sana kwenye mchezo mmoja wa Champions League msimu huu.

Kifuatacho?

Manchester City haitokuwa na mchezo mwishoni mwa wiki hii kwa sababu Manchester United itakuwa kwenye fainali ya League Cup hivyo kuufanya mchezo wa Manchester kughairishwa, hivyo mechi yao inayofuata itakuwa FA Cup raundi ya tano marudiano na Huddersfield katika dimba la Etihad Jumatano, 1 Machi.
Monaco, kwa upande wao, watakuwa ugenini dhidi ya Guingamp Jumapili wakitazamia kuimarisha uongozi wao wa Ligue 1.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.