Online

Wednesday, February 15, 2017

UEFA: Paris St-Germain 4-0 Barcelona: Angel di Maria apiga mbili, Barca ikifa Ufaransa

Angel di Maria alifunga mara mbili Paris St-Germain ikiichapa Barcelona mabao 4-0 na kuiweka timu hiyo kwenye hatari ya kukosa robo-fainali ya Champions League kwa mara ya kwanza katika muongo mmoja.
PSG ilitawala mchezo huu wa kwanza raundi ya 16 na ikapata bao la kuongoza kupitia kwa Di Maria aliyefunga kwa free-kick.
Julian Draxler akaongeza bao la pili kabla ya Di Maria kufunga bao la tatu.
Edinson Cavani akafunga bao la nne.
Timu ya Barcelona - ikiwa na nyota wake Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar mbele - haikuwa na kiwango bora kama ilivyo siku zote na hawakuwa na athari zozote mpaka pale zilizposalia dakika saba mchezo kumalizika baada ya Samuel Umtiti kupiga kichwa kilichogonga nguzo.
Kichapo hicho kinaiacha timu ya Luis Enrique katika hatihati ya kuondolewa mashindanoni watakapoialika PSG kwenye mchezo wa marudiano 8 Machi.
Hakuna timu iliyowahi kurudisha mabao manne ya mchezo wa kwanza kwenye historia ya Champions League.

Barca yapata kichapo kikubwa zaidi - dondoo

  • Paris St-Germain inakuwa timu ya sita kufunga mabao manne  kwenye mchezo wa Champions League vs Barcelona (baada ya Milan, Dynamo Kiev, Valencia, Chelsea na Bayern Munich).
  • Hasa, hiki kilikuwa kichapo kikubwa sana kwa Barcelona kwenye mashindano haya (0-4 vs Milan mwaka 1994, Dynamo Kiev mwaka 1997 na Bayern Munich mwaka 2013).
  • Angel Di Maria amefunga mabao manne kwenye Champions League msimu huu - mabao mengi kwenye msimu mmoja.
  • Ni Lionel Messi (10) pekee amefunga mabao mengi zaidi kwenye Champions League msimu huu zaidi ya Edinson Cavani (saba).
  • Hakuna timu iliyowahi kufungwa mabao 4+ ikarudisha na kusonga mbele kwenye mtoano wa Champions League.
  • Barca ilikumbana na mashuti 10 yaliyolenga lango vs PSG - mengi zaidi kwenye mechi moja ya Champions League tangu msimu wa 2003-04 (pia vs Bayer Leverkusen Disemba 2015).

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.