Online

Wednesday, February 15, 2017

UEFA: Real Madrid v Napoli: Cristiano Ronaldo yuko fit kujenga heshima ya Zidane

Cristiano Ronaldo amepona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua na atajumuishwa kwenye kikosi cha Real Madrid ambacho kitakuwa Santiago Bernabéu kupepetana na Napoli kwenye mchezo wa kwanza wa Champions League hatua ya mtoano Jumatano usiku.
Fowadi wa Ureno alikosa mazoezi Jumatatu baada ya kupata majeraha madogo katika mchezo wa Jumamosi ambao Madrid walishinda dhidi ya Osasuna kwenye La Liga.
Hata hivyo, winga wa Wales Gareth Bale (enka) hatocheza.
Mshambuliaji Arkadiusz Milik yuko fit kwa Napoli.
Mshambuliaji huyo wa Poland amepona majeraha yake na amejumuishwa kwenye kikosi cha miamba hiyo ya Serie A. Mlinzi Lorenzo Tonelli, ambaye hajacheza tangu 21 Januari, pia amesafiri na timu.
Mchezo mwingine utapigwa Allianz Arena ambapo Arsenal watakuwa wageni wa Bayern Munich.

Zidane kuwakabili Napoli wazuri

Mabingwa watetezi Real Madrid wanapanga kutinga robo-fainali ya Champions League kwa mara ya sababmfululizo.
Napoli, wakati huo huo, ipo kwenye hatua ya mtoano kwa mara ya pili pekee lakini kocha wa Real Zinedine Zidane hachukulii mambo kuwa rahisi namna hiyo dhidi ya timu hiyo kutoka Italia.
"Huwezi kushinda mtoano kwa mchezo mmoja," alisema. "Tunakwenda hatua kwa hatua na mchezo kwa mchezo.
"Kila mmoja anataka kushinda Champions League lakini ni barabara ndefu na ngumu tuliopo.
"Napoli ni timu inayoshambulia vizuri na kucheza kwa kasi kubwa. Ni wafupi, wachezaji wanaojua wakifanyacho akiwa na mbinu nzuri.
"Tuna zana za kuwafanya waumie na tunataka kufanya hivyo."

Napoli inaweza kuwafunga mabingwa wa dunia?

Vinara wa La Liga Real wamepoteza mara mbili pekee msimu huu - dhidi ya Sevilla kwenye ligi 15 Januari na dhidi ya Celta Vigo kwenye Copa del Rey siku tatu baadaye.
Napoli, wakati huo huo, inaingia uwanjani kwenye mchezo huu wakiwa na kiwango kizuri, wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja kwenye mechi 18 tangu Oktoba.
"Kwa tahadhari kwamba tunacheza ugenini dhidi ya mabingwa wa dunia na timu ngumu hasa, tutakuwa na hofu kidogo," alisema kocha wa Napoli Maurizio Sarri.
"Wakati mwingine ni hisia chanya kwa sababu inakupa nguvu. Upande mwingine kama hauna hamasa kupambana na mpinzani wako kwa uelekeo hakuna hitajio la kucheza."

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.