Online

Friday, February 3, 2017

VPL: Mechi za wikiendi hii Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo Februari 3, kwa mchezo mmoja ambapo mabingwa watetezi Young Africans watakuwa wenyeji wa Stand United ya Shinyanga kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Ligi hiyo itaendelea Jumamosi Februari 4, kwa mechi mbili ambapo Wagonga Nyundo wa jiji la Mbeya, Mbeya City Council F.C wakiwakaribisha JKT Ruvu kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mchezo mwingine utapigwa kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea ambapo 'Wana Lizombe' Majimaji FC wakiwa wenyeji wa Simba SC.
Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Ndanda FC kwenye uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam – mchezo unaotarajiwa kuanza saa 1.00 usiku.
Aidha, Jumatatu kutakuwa na mchezo mmoja ambao utazikutanisha Toto Africans ya Mwanza dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.