Online

Wednesday, January 17, 2018

KITAIFA: Agizo jingine President JPM kalitoa kwenye Elimu leo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za Msingi na Sekondari na hataki kusikia kuwa wanafunzi wanarudishwa shuleni kwa ababu hawajalipa mchango wa chakula au dawati.

President JPM amewataka Mawaziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na TAMISEMI Selemani Jafo kulisimamia hilo huku akiwaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi nchi nzima kuhakikisha hakuna Shule ambayo inachangisha mchango wa aina yoyote huku akisema kwa yeyote atakataka kuchangia basi apeleke mchango wake kwa Mkurugenzi ambaye ataamua matumizi ya mchango huo kwa shule husika.


No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.