Online

Thursday, June 7, 2018

POLISI MTWARA: Yawakamata waliotoa HUNDI HEWA kununua PetrolJESHI la Polisi mkoani Mtwara linawashikilia watu 15 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya wizi wa pikipiki na kutoa hundi hewa yenye thamani ya Tsh 9,450,000.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mkoani humo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amesema kati ya May 27 na June 5, 2018 katika operesheni ya kukamata Wahalifu mkoani humo, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukamata pikipiki 7 za wizi aina mbalimbali pamoja na watuhumiwa 11 kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

RPC Mkondya ameongeza kuwa, watuhumiwa wanne kati yao na pikipiki mbili wamekamatwa Wilayani Tandahimba katika kijiji cha Maundo wakati watuhumiwa saba na pikipiki tano wamekamatwa katika Wilaya ya Mtwara Vijijini katika vijiji vya Mpapura, Kitere, Namgogori, Mabatini-Mpapura na Utendea ambapo watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Aidha, katika tukio lingine, RPC Mkondya amesema Jeshi hilo linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kutoa hundi hewa yenye thamani ya Tsh 9,450,000 kwa lengo la kununua lita 4,000 za mafuta ya Petrol katika kituo cha Mafuta Ufukoni kilichopo Mtwara Mjini. Upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea na watuhumiwa watafikishwa Mahakamani pindi utakapokamilika.No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.