Online

Sunday, August 12, 2018

PICHA 10: Linavyoonekana jumba la USHER RYMOND linalouzwa Tsh BILIONI 7

STAA wa RnB kutoka Marekani Usher Rymond ameliingiza sokoni kwa mara ya pili jumba lake la kifahari baada ya mara ya kwanza kukosa mteja.

Mtandao wa Los Angeles Times umeripoti kuwa jumba hilo linauzwa dola MILIONI 3.75 ambazo ni zaidi ya Tsh BILIONI 7.  

Usher mwenye miaka 39 amekuwa akilimiki jumba hilo lenye vyumba vitano vya kulala tangu mwaka 2015.

Jumba hilo lina eneo la futi 4,261, likiwa na vyumba vitano vya kulala ambapo awali aliliingiza sokoni mwezi February akiliuza dola MILIONI 4.2 zaidi Tsh BILIONI 8. 


No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.